Bibilia inasema nini kuhusu vita vya kiroho?
Kuna makosa mawili ya kimsingi wakati inafikia vita vya kiroho-kutilia mkazo sana, na kukosa kutilia mkazo. Wengine wanalaumu kila aina ya dhambi, kila mgogoro, na kila shida kwa mapepo ambayo yanastahili kukemewa. Wengine kabisa wanapuuza ulimwengu wa kiroho na dhana kwamba Bibilia inatuambia kwamba vita vyetu ni kupigana na nguvu za giza. Ufunguo wa ufanisi wa vita vya kiroho ni kupata usawa wa bibilia. Yesu wakati mwingine aliyakemea mapepo na wakati mwingine aliwaponya watu bila kutaja mapepo. Mtume Paulo aliwaamuru Wakristo kupigana vita na dhambi zilizo ndani yao (Warumi 6) na kupigana vita na yule mwovu shetani (Waefeso 6:10-18)
Waefeso 6:10-12 yasema, “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Ujumbe huu wafunza baadhi ya kweli muimu: tutaweza kuwa na uwezo kwa nguvu za Mungu, ni silaha ya Mungu ambayo yatulinda, na vita ni kupinga na nguvu za giza za ulimwengu huu.
Mfano wa nguvu sana juu ya ngunvu za Bwana ni ule wa malaika Mikaeli katika Yuda 9. Mikaeli ambaye ni mwenye nguvu zaidi ya malaika wote wa Mungu, hakumkemea Shetani kwa nguvu zake, bali alisema, “Mungu anakukemea!” Ufunuo 12:7-8 yanakiri kwamba katika nyakati za mwisho Mikaeli atamshinda Shetani. Bado, wakati inafikia mapigano yake na Shetani, Mikaeli alimkemea Shetani katika jina la Mungu na mamlaka yake, si kwa nguvu zake. Ni kupitia kwa uhusiano wetu na Yesu Kristo kuwa Wakristo wako na mamlaka yoyote juu ya Shetani na mapepo yake. Ni kupitia kwa jina lake kuwa kemeo letu liko na nguvu.
Waefeso 6:13-18 yatupa elezo la silaha za kiroho Mungu anapeana. Tunastahili kusimama dhabiti na kufunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kufuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani, kuchukua ngao ya wokovu na kwa kuomba katika roho. Je! Inamaanisha nini kuwa sehemu za silaha za roho zinawakilisha katika vita vya kiroho? Tunastahili Kunene ukweli tukipinga ujanja wa Shetani. Tunastahili kutia nanga katika dhana kuwa tumetangazwa kuwa watakativu kwa sababu ya kusulubiwa kwa Kristo kwa ajili yetu. Tunastahili kuitangaza Injili, hata kama tutapata pingamizi. Hatustahili kuyumbayumba katika imani yetu, uakikisho wetu kwamba hakuna nguvu zozote za giza zitakzo tushinda. Silaha yetu ya kupinga ni Neno la Mungu, sio maoni yetu na hisia zetu. Tunastahili kufuata mfano wa Yesu kwa kutambua kuwa ushindi unawezekana kupitia kwa maombi.
Yesu ndiye mfano wetu pekee katika vita vya kiroho. Tazama vile Yesu alikabiliana na mitego kutoka kwa Shetani wakati alijaribiwa na Shetani jangwani (Mathayo 4:1-11). Kila jaribu lilijibiwa njia ile ile kwa maneno “Imeandikwa.” Yesu alijua neno la Mungu kuwa silaha yenye nguvu kupingana na majaribu ya Shetani. Ikiwa Yesu mwenyewe alitumia Neno kukabili Shetani, je! Tunastahili kutumia kitu kingine tofauti?
Mfano hatimaye wa jinsi ya kupigana vita vya kiroho ni wa wana saba wa Skewa. “Baadhi ya Wayaudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, Yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? na Yule mtu aliyepagwa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa” (Matendo Ya Mitume 19:13-16). Wele wana saba wa Skewa walikuwa wakitumia jina la Yesu. Hiyo haitoshi. Wale wana saba wa Skewa hawakuwa na uhusiano na Yesu; kwa hivyo, maneno yao yalikuwa matupu kwa nguvu yoyote au mamlaka yoyote. Wale wana saba wa Skewa wilikuwa wakitegemea utaratibu/methodolojia. Hawakuwa wakimtegemea Yesu kama Bwana na mwokozi wao, na hawakuwa wakitumia neno la Mungu katika vita vyao vya kiroho. Kwa sababu hiyo, wakapokea kichapo cha kuaibisha. Na tujifunze kutoka kwa mfano huu na mienendo ya vita vya kiroho vile Bibilia inatamuru.
Kwa ufupi, njia za ufanisi wa vita vya kiroho ni zipi? Kwanza, tunategemea nguvu za Mungu, sio nguvu zetu. Pili, tunakemea kwa jina la Yesu, sio kwa jina letu. Tatu, twajikinga kwa kuvaa silaha zote za Mungu. Nne, twapigana vita kwa upanga wa roho-Neno la Mungu. Mwisho, tunakumbuka kwamba, tunapopigana vita vya kiroho na Shetani na mapepo yake, sio kila dhambi au taabu ni pepo ambayo yahitaji kukemewa.
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili
Bibilia inasema nini kuhusu vita vya kiroho?
ncG1vNJzZmivp6x7qLvTqqyeq6SevK%2B%2FjaipoGd7nsC4rceio6Jnpp7BonnVsphmo5mnvKm7jaGrpqQ%3D